Mkurugenzi Ajira Zanzibar Mr. Ameir A. Ameir (Aliesimama) akiwandaa Vijana kukabiliana na Usaili

Kutokana na ukosefu wa vijana kujiamini hasa wakati wa usaili Wizara ya Kazi, Uweseshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar kupitia Idaraya Ajira imekua ni sualal la kawaida kuwapatia mafunzo vijana mara kwa mara juu ya hali halisi ya soko la ajira na changamoto zake, imeonekana wazi kuwa vijana walio wengi wana ujuzi wa kutosha lakini wanakosa kujiamini hasa wakati wa usaili jambo ambalo limeipelekea Idara ya Ajira kuchukua juhudi za makusudi katika kuwajenga Vijana juu ya kupambana na uzaifu huo waliokua nao na wakati mwengine Idara hii huwafunza vijana kivitendo zaidi namna ya kuwakabili waajiri mbalimbali ikiwemo wageni au wazawa lengo ikiwa ni kuwapika vijana na kuwapa fursa ya kukutana na waajiri hao.